Friday, 4 December 2015

WAWILI WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI ILIYOBEBA MAGAZETI YA MWANANCHI


GARI iliyokuwa imebeba magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti ikitokea Dar es Salaam kuelekea Iringa na Mbeya, imepata ajali katika mlima wa Kitonga, wilayani Kilolo mkoani Iringa leo alfajiri.

Watu wawili wamekufa papo hapo na wengine sita kujeruhiwa, mmoja vibaya baada ya gari lililokuwa likisafirisha magazeti ya mwananchi kutoka Dar es Salaam kwenda Iringa  na Mbeya  kupata ajali eneo la mlima kitonga barabara kuu ya Dar-es-Salaam-Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 11 alfajiri gari hilo la magazeti kuingia nyuma ya roli likiwa katika mwendo kasi.

“Leo imetoka ajali mbaya sana hapa Iringa, ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Haice iliyokuwa imebeba magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communication LTD; gari hilo lilipata ajali baada ya kuganga lori lenye tela kwa nyuma:

“Dereva wa gari  hilo lililopata ajali alitaka kulipita roli ambalo nalo lilikuwa linaelekea Mbeya; alipokuwa akitaka kulipita aliona gari likija mbele yake na wakati akifanya maamuzi ya kurudi upande wake aligonga roli hilo kwa nyuma,”alisema.

Mungi aliwataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Eliud Ogwasa (40) na Godfrey Owino (34) wote wakazi wa mkazi  Dar es Salaam.

Aliwataka majeruhi kuwa ni Baraka Shitindi (32) ambaye hali yake ni mbaya na Kevin Shitindi (30) wakazi wa Mbozi Mkoani Mbeya na Herold Shitindi (25) mkazi wa Morogoro.

Wengine ni  Zabroin Izote (29) mkazi wa mbeya na Joseph Kayani (37) mkazi wa Mafinga mkoani Iringa.

“Kamanda Mungi aliwaasa madereva kuwa makini na kuendesha gari kwa kuzingatian sheria za barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuwapotezea maisha wao na abria wao,” alisema.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa Alfred Mwakalebela alisema wamepokea maiti mbili ambazo wamehifadhi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo.

Dkt. Mwakalebela alisema pia wamepokea majeruhi wanne ambao wameumia maeneo mbalimbali mwilini ikiwemo kuvunjika mguu huku mmoja kati yao akiwa na hali mbaya zaidi kiasi cha kushindwa kuzungumza.

Majeruhi Kevin Shitindi ambaye ambaye ameumia mkono na kifuani alisema walitoka Dar es Salaam saa sita usiku wakiwa 10 kwenye gari hiyo na walipofika Morogoro saa nane watu wawili walishuka.


Majeruhi Kayani na Lisote walisema hiace hiyo ilikuwa inakwenda kasi na wakati ajali inatokea wao walikuwa wamelala walichosikia ni kishindo na baadaye kuona madereva wamekufa papo hapo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment