Monday, 21 December 2015

VIJANA WA CCM WAJITOKEZA KUMPA ULINZI MWENYEKITI WA CCM MKOA WA IRINGA AWAPO KWENYE MAJUKUMU YAKE KICHAMA
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jesca Msambatavangu leo hii ameingia katika ofisi za CCM Mkoa wa Iringa akiwa kifua mbele baada ya vijana wanaomuunga mkono kujitokeza kwa wingi na kumuhakikishia usalama wake katika kipindi chote alichopanga kuwepo katika ofisi hizo.

Msambatavangu anayetuhumiwa kukihujumu chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, Jimbo la Iringa Mjini alifika katika ofisi hizo majira ya saa nne asubuhi na akaendelea kuwepo hapo mpaka majira ya saa 11 jioni.

Akiwa ofisini kwake, Msambatavangu alitumia fursa hiyo kuzungumza na vijana hao juu ya kile alichodai kinafanywa dhidi yake na kiongozi mwenzake wa chama hicho mkoani Iringa ikiwa ni siku mbili tu baada ya kufungiwa ndani ya ofisi hizo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza na wajumbe wengine wa Kamati ya Siasa ya Mkoa.

Vijana hao walimfungia katika ofisi hizo wakishinikiza ajiuzulu kutokana na tuhuma hiyo ya usaliti iliyopelekea jimbo hilo la Iringa Mjini lichukuliwe kwa awamu nyingine ya miaka mitano na Mchungaji Peter Msigwa ambaye chama chake, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilinyakua pia kata 14 kati ya 15 za udiwani.

Baada ya kumaliza kikao na vijana hao walioongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Manispaa ya Iringa, Kaunda Mwaipyana, Msambatavangu alizungumza na wanahabari na kueleza muelekeo wa chama hicho jimbo la Iringa Mjini na mkoani Iringa kwa ujumla wake.

Taarifa hii itakujia kwa kina hivipunde, endelea kutufuatilia………………………….

Reactions:

0 comments:

Post a Comment