Wednesday, 16 December 2015

UMMY MWALIMU AWASHITUKIZA MUHIMBILI, AKUTA MASHINE ZA CT SCAN NA MRI HAZIFANYI KAZI TOFAUTI NA MAAGIZO YA RAIS

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu akimsalimia mmoja wa mama aliyelazwa katika Hospitali moja hapa jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu ameendelea na ziara ya kushitukiza ambapo leo amefika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Katika Hospitali hiyo amejionea mashine za CT Scan na MRI zikiwa hazifanyi kazi licha ya Rais Dk John Magufuli kuitaka Hospitali hiyo kuhakikisha kuwa mashine hizo zinafanya kazi ipasavyo.

Kwa upande wake  Mkurugenzi Wa Hospitali hiyo, Lawrence Museru amesema  mashine hizo ziliharibika tangu juzi na hivyo huduma zilisimama tangu jana asubuhi hadi leo.

Amesema tatizo kubwa katika machine ya CT Scan picha hazisomeki vizuri na MRI imeharibika na akaahidi kwamba matengenezo  yake yataanza kufanywa leo.

Mwalimu ameutaka  uongozi wa hospitali hiyo  kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kuwa mashine hizi zinarudi katika hali yake ya kawaida.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment