Monday, 21 December 2015

UKAWA WAJITOSA SAKATA LA UFUKWE WA COCO, MKURUGENZI KUNG'OLEWA

Mbunge wa Ubungo Said Kubenea.

Sakata la uuzaji ufukwe wa Coco uliopelekea pia aliyekuwa Mkurungenzi wa Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty kusimamishwa kazi limechukua sura mpya baada ya madiwani wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa) kupinga kusimamishwa kwa mkurugenzi huyo.

Pamoja na sababu zingine, Natty alisimamishwa kazi akituhumiwa  kushindwa kusimamia vyema mkataba wa ubinafsishaji wa ufukwe huo kwa mfanyabishara Yusuf Manji.

Wakizungumza na wanahabari, madiwani hao wamesema Mhandisi Natty alisimamishwa kazi kwa sababu za kisiasa ikiwemo kutenda haki wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, hali iliyoisaidia Ukawa isidhurumiwe haki yake.

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea pamoja na Boniphace Jacob (Chadema) walionesha mikataba  iliyoingiwa kati ya Manispaa ya Kinondoni na Yusuph Manji  ambayo wamedai wakati ikisainiwa Natty hakuwepo.

Kwa upande mwingine madiwani hao wametaka serikali  iunde Tume kwa ajili ya kubaini ukweli katika sakata  hilo, tume   ambayo  haitwahusisha Tamisemi na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

 chanz; hivisasa blog

Reactions:

0 comments:

Post a Comment