Tuesday, 8 December 2015

TAMASHA LA MICHEZO LAWAKUTANISHA 150 WA AFRIKA MASHARIKI


ZAIDI ya vijana 150 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati wanatarajia kushiriki katika tamasha la mpira wa miguu la kimataifa lijulikanalo kama ‘SOCCER FOR PEACE’ linalolenga kuhamasisha vijana kushiriki katika mchakato wa kuhamasisha amani na maendeleo kwa watu wote.

Tamasha hilo litakalofanyika kwa wiki moja mjini Iringa kwa uratibu wa  asasi ya STREET FOTBALL WORLD linalojumisha mashirika zaidi ya 100; linalojumuisha vijana wa kike na kiume wa kati ya miaka 14 hadi 17 kutoka mashirika 16  yenye lengo la kutumia michezo kufanya kazi hiyo.

Akizungumza na wandishi wa habari katika uwanja wa kimataifa wa FIFA
mjini hapa mwenyekiti  wa kongamano hilo kutoka nchini Kenya, Gishuku
Fransis alisema kwa kutumia michezo ni rahisi kuwafundisha watoto wadogo kudumisha amani.

“Watoto wakifundishwa kupendana toka ujana wao, hakuna nchi ingekuwa na vita, chakushangaza baadhi ya nchi kuna watoto wanatumiwa katika vita,” alisema.

Mkurungenzi wa Shirika lisilo la Kiserekali la IDYDC, Dk John Mkoma ambao ni wenyeji wa tamasha hilo alisema ; “mashindano haya yameletwa nchini ikiwa ni hatua mojawapo ya kuenzi utamaduni wa watanzania na kuuonyesha ulimwengu jinsi tunavyoweza kulinda  na kudumisha Amani yao.”


Nkoma alisema kwa kupitia tamasha hilo la michezo, vijana watajifunza mambo mbalimbali yanayohusu amani, maendeleo na michezo.

Ili kuizoea dhana ya amani, vijana wanaoshiriki tamasha hilo watajisimamia wao wenyewe katika mahindao watakayofanya.

Wanafunzi wanaoshiriki tamasha hilo wamewashauri wazazi kujenga utamaduni wa kuwaruhusi kushiriki katika michezo ili kujenga afya ya mwili na akili lakini pia na kuibua vipaji vyao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment