Wednesday, 16 December 2015

SIMBACHAWENE AKERWA NA UCHAFU ULIOKUSANYWA SIKU YA UHURU

Rais John  Magufuli alipokuwa akifanya usafi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurungenzi wote wa halmashari nchini kuhakikisha wanazoa taka zote zilizokusanywa wakati wa siku ya uhuru kabla ya tarehe 20 mwezi huu.

Akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha kumkaribisha katika ofisi ya Tamisemi mjini Dodoma Simbachawene amesema hataki kuona uchafu uliokusanywa siku ya uhuru ukiendelea kuonekana katika maeneo uliokusanywa.

Waziri huyo  amewataka pia watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wa kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kuwa  awamu ya tano haitaendelea kuwalea watendaji wa aina hiyo.

Naye Naibu Waziri wa wizara hiyo Suleiman Jaffo, amewataka watumishi hao kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuweza kuboresha maisha ya wananchi.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment