Monday, 21 December 2015

RAIS MAGUFULI NA MAALIM SEIF WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais Magufuli amekutana na kuzungumza na mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif juu ya mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar

Picha ya pamoja ya Maalim Seif,Rais Dkt John Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu.

Rais Dk John Magufuli amekutana na kuzungumza na aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad juu ya mgogoro wa uchaguzi mkuu wa Rais wa visiwa hivyo unaoendelea kufukuta chini chini.

Mkutano baina ya viongozi hao umefanyika ikiwa ni siku kadhaa tangu Bodi ya MCC kutangaza kusitisha msaada wa dola Milioni 472.8 ambazo ni sawa na takribani Sh Trillion Moja kwasababy ya mgogoro huo.

Fedha hizo zililenga kusaidia sekta ya nishati ya umeme hususani ule wa vijijini kwa kuunganisha wateja wapya, na kufanya mabadiliko ya kimuundo ya Shirika la Umeme (Tanesco) ili lifanye kazi na kutoa huduma kwa ufanisi katika sehemu za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji.

Fedha hizo pia zilikusudiwa kusaidia kuanza kwa mpango mkubwa wa kuboresha sekta ya umeme nchini 2014-2024.

Mazungumzo ya viongozi hao wawili yamehudhuriwa pia na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Viongozi hao kwa pamoja wamejadili hali ya kisiasa Zanzibar na wamaefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea.

Rais Dk Magufuli ameamuahidi Maalim Seif kwamba mazungumzo yataendelea hadi suluhisho la kisiasa litakapopatikana.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment