Monday, 7 December 2015

RAIS AWAFUTA KAZI KATIBU MKUU UCHUKUZI, MKURUGENZI NA MWENYEKITI WA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

RAIS John Magufuli ameivunja kuanzia leo iliyokuwa bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kumsimamisha kazi aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa TPA pamoja na kutengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi.

Mbali na maamuzi hayo ya Rais lakini Pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza  kuwasimamisha kazi watumishi nane na viongozi wa TPA.

Kutokana na utendaji mbovu wa mamlaka ya Bandari Tanzania kwa muda mrefu na kwa kitendo cha kutochukua hatua kwenye vyanzo, Rais Mgufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa bodi ya TPA, Prf. Joseph Msambichaka pamoja na uteuzi wa Mkurugenzi wa TPA, Awadh Massawe.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema wakati wa ziara yake TPA alitoa maagizo mfumo wa malipo bandarini ubadilike kutoka billing system na uwekwe mfumo wa e-payment na uwe umekamilika ifikapo Desemba 11, mwaka huu.

“Kwakuwa ripoti iliwataja waliohusika na upitishaji wa makontena na hakuna hatua iliyochukuliwa, kuanzia muda huu nawasimamisha kazi wale wote waliohusika kupitisha makontena kinyume na utaratibu,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Majaliwa aliwataja watu hao kuwa ni Wasimamizi wa bandari Kavu (ICD) Happygod Naftari, Juma Zaar, Steven Naftari Mtui, Titi Ligalwike, Lydia Prosper Kimaro, Mkango Alli, john Elisane na James Kimwomwa ambaye alihamishiwa Mwanza.

Aidha aliwataja viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa ya makontena kutoka ndani ya bandari ambao hawamo kwenye ripoti ila ni wahusika wakuu kuwa ni pamoja na Aliyekuwa meneja Mapato akahamishiwa makao Makuu kitengo cha Fedha, Shaban Mngazija, Aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa bandari Kavu (ICD) ambaye amehamishiwa Makao Makuu kwa Naibu Mkurugenzi wa Co-oparate Service , Rajab Mdoe.

Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Ibin Masoud, Meneja Bandari Msaidizi Fedha, Apolonia Mosha na James Kimwomwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment