Sunday, 27 December 2015

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA IRINGA NA WENGINE WALIOTAJWA KUKISALITI CHAMA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU KUANZA KUHOJIWA


KAMATI za Maadili za Chama cha Mapinduzi (CCM) za ngazi mbalimbali mkoani Iringa zinaanza kukutana Jumatatu ya Desemba 28 kusikiliza ushahidi toka kwa wana CCM wanaodaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Mmoja wa watakaoitwa na kamati hizo ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu na Mjumbe wa Halmashauri ya CCM Taifa, Mahamudu Madenge.

Msambatavangu na Madenge wanatuhumiwa pamoja na wasaliti wengine 30 wa mjini Iringa kukisaliti na kukihujumu chama hicho hadi kikapoteza ubunge kwa mara nyingine tena kwa Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema na kikanyang’anywa kata 14 walizokuwa wakizishikiria kwa miaka yote.

Kwa upande wake, Msambatavangu ambaye mara kwa mara amenukuliwa akipinga kuhusika katika tuhuma hizo, amesema yupo tayari kutoa ushirikiano kwa kamati hizo na akawataka watuhumiwa wengine wafanye hivyo ili kumaliza suala hilo linalozidi kukigawa chama hicho mkoani hapa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment