Thursday, 17 December 2015

MUFINDI YAONGOZA MKOANI IRINGA KWA MAANDALIZI BOMBA YA MBIO ZA MWENGE


Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa imeibuka mshindi wa kwanza kimkoa na kushika nafasi za juu kikanda na kitaifa, baada ya kufanya vizuri zaidi wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru ulipokimbizwa Mkoani Iringa, Juni mwaka huu.
   
Taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri hiyo imesema kulikuwepo na vigezo 10 vilivyotumika kuwashindanisha na akavitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na uzinduzi wa miradi yenye maslahi kwa umma, na uimarishaji wa vikundi vya uzalishaji mali kwa wanawake na vijana.

Vingine ni pamoja na mapambano dhidi ya Malaria, dawa za kulevya, michango ya Mwenge na mapokezi ya mwenge huo ulipowasili wilayani humo. 

Akizunguzia ushindi huo, Mkuuwa wilaya ya Mufindi JOWIKA KASUNGA amewashukuru wakazi wa Mufindi na wadau wa maendeleo kwa michango yao na akatoa rai ya kundelea kuuenzi mwenge huo kama alama na utambulisho wa Taifa.

Aidha, taarifa hiyo imezitaja nafasi ilizoshika kuwa ni ushindi wa kwanza kimkoa, ushindi wa 05 kwa kanda ya kiuchumi yenye zaidi Halmashauri 36 pamoja na nafasi ya 22 kitaifa ikijumuisha zaidi ya Halmashauri 140.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment