Thursday, 24 December 2015

MTENDAJI MKUU WA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI APIGWA CHINI

Mtendaji Mkuu wa DART, Bi. Asteria Mlambo akihojiwa na vyombo vya habari.

Kasi ya Rais John Pombe Magufuli imeendelea kuwang’oa watendaji mbalimbali katika idara za serikali wanaotuhumiwa kwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za umma.

Jana timua timua ya serikali ya Dk Magufuli ilimkumba Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (DART) jijini Dar es Salaam, Asteria Mlambo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene amesema  amemsimamisha kazi Asteria baada ya kubainika kushindwa kuzingatia Sheria ya Manunuzi ya Umma wakati wa kumpata mtoa huduma katika kipindi cha mpito.

Simbachawene amesema mtendaji huyo alishindwa kuchukua hatua hata pale alipobaini kuwa mtoa huduma wa mpito amekiuka masharti ya mkataba wa kutoa huduma ya mpito na kufanya maamuzi makubwa pasipo kuishirikisha Bodi ya Ushauri ya DART.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment