Wednesday, 30 December 2015

MOROGORO KUJENGA SOKO KUU LA KISASA, NI BAADA YA FEDHA KUPATIKANA


 UJENZI wa soko kuu litakalokuwa la  kisasa katika   Manispaa ya Morogoro unatarajia kuanza wakati wowote  ule baaada ya kukamilika kwa michoro ya soko hilo.

Aidha awamu ya kwanza ya fedha za ujenzi kiasi cha  Sh bilioni 10,  kati ya bilioni 19.3, imeelezwa zimeshapatikana.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Theresia Mahongo,amethibitisha kwamba ramani ya michoro ya ujenzi wa soko ameshakabidhiwa kwa hatua nyingine.

Awamu ya kwanza itatumia sh bilioni 10; saba zikiwa za mkopo kutoka  benki na nyingine kutoka vyanzo wa mapata ya Halmashauri ya Manispaa hiyo.

Licha ya michoro kuandaliwa, baadhi ya wadau na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Manispaa hiyo waliozungumza kwa nyakati tofauti walishauri Uongozi wa Manispaa kukafikiria kujenga soko lenye ghorofa zaidi ya sita kwa kuangalia mahitaji ya sasa na  miaka mingine  ijayo.

Walisema kuwa, ghorofa nyingine za zinaweza kuwa ni maegesho ya magari kwa kutozwa  ushuru utakaoongeza mapato ya  halmashauri badala ya mpango wa sasa wa kujenga soko la ghorofa moja ambalo halitakidhi mahitaji ya baadaye ya ukuaji wa Manispaa hiyo.

Soko kuu linalotumika kwa hivi sasa lilijengwa  mwaka 1953 na wakoloni na limekuwa ni chakavu kupindukia huku likizidiwa na uwepo wa idadi kubwa ya wafanyabiashara.

Reactions:

1 comments:

  1. kiongozi tusaidie mchoro wa soko kama unapatikana

    ReplyDelete