Monday, 7 December 2015

LOWASSA KUMPIGA TAFU GODBLESS LEMA UCHAGUZI WA UBUNGE ARUSHA MJINI

Aliyekuwa Mgombea Urais wa Chadema Edward Lowassa.

VITA ya Ubunge jimbo la Arusha Mjini kati ya Mgombea wa Chadema Godbless Lema anayetafuta kutetea kiti hicho na yule wa CCM Phillemon Mollel; inatarajia kunoga zaidi wiki hii baada ya kuwepo kwa taarifa za baadhi ya vigogo wa vyama hivyo kutua katika jiji hilo ili kuwapiga tafu wagombea wao.

Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo, haukufanyika Oktoba 25 mwaka huu kama ilivyokuwa kwa majimbo mengine nchini baada ya mgombea wa ACT Wazalendo Estomiah Mallah kufariki dunia.

Huku kukiwa hakuna uhakika wa nani kati ya vigogo wengi wa CCM watakwenda jijini Arusha kumpiga tafu mgombea wao, kwa upande wa Chadema aliyekuwa mgombea urais wa Chadema , Edward Lowassa anatarajia kuanza kukampeni bega kwa bega na mgombea wa chama chake, Lema.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa jijini Arusha, wanasema itakuwa ngumu sana kwa mgombea wa CCM, Mollel kumuangusha Lema katika kinyang’anyiro hicho japokuwa wengine wanasema lolote linaweza kutokea.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment