Monday, 21 December 2015

KITWANGA ATANGAZA KUPAMBANA NA MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA

Waziri wa Mambo ya ndani Charles Kitwanga akizungumza na Waandishi wa Habari.

Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchini, Charles Kitwanga ametaja  hatua itakayosaidia  katika kupambana  na dawa za kulevya nchini  ikiwemo uingizaji pamoja na usambazaji wake.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo  Kitwanga amesema watabuni mfumo utakaosadia kudhibiti uingizwaji wa dawa hizo nchini, kuvunja mtandao wa dawa hizo na kuwakamata wahusika wote wa biashara hiyo na kuwafikisha katika vyombo vya dola.

“Na tutasaka na kukamata dawa zote zilizopo nchini, kuwakamata wahusika wake na kuwafikisha mahakamani ,” alisema.

Katika hatua nyingine, Kitwanga amesema serikali imeanza kulifanyia kazi suala la kuimarisha ulinzi katika bandari zake zote nchini kwa kuweka askari wa kutosha kwa kadri inavyohitajika.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment