Tuesday, 8 December 2015

KASI YA MAGUFULI YATUA MKOANI KATAVI, DED NA MAAFISA WENGINE 10 WA HALMASHAURI YA MPANDA WASIMAMISHWA KAZI

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk Ibrahim Msengi.

KASI ya Rais John Magufuli kuwatimua watendaji wazembe imetua mkoani Katavi na kuoneshwa na mkuu wa mkoa huo, Dk Ibrahim Msengi aliyetangaza kuwasimamisha kazi maofisa waandamizi 11 wa Manispaa ya Mpanda akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wake, Suleiman Lukanga kwa ukiukwaji wa sheria za manunuzi unaowahusisha na tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 92.8.

Mkurugenzi huyo  pamoja na  maofisa 11 wa Manispaa ya Mpanda wanatuhumiwa kununua gari la hewa la kubeba taka kwa kiasi cha Sh milioni 92.8 zinazopnesha zililipwa kwa kampuni hewa.

Wengine waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Vincent Kayombo ambaye pia ni Ofisa Elimu (Msingi) wa Manispaa ya Mpanda, Ofisa Manunuzi aliyetajwa kwa jina moja la Kakulima.

Wengine ni  Ofisa Mipango, Ferdinard Filimbi, Mweka Hazina, Bosco Kapinga, Mhasibu Kibi Hamis Msaka na wajumbe wanne wa Bodi ya Zabuni.

Aidha, Dk Msengi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo, ameamuru wakati uchunguzi kuhusu tuhuma hizo ukiendelea, watuhumiwa wote 12 wasitoke nje ya Mji wa Mpanda na wahakikishe wanalipa kiasi hicho cha fedha kwa kuwa ni fedha za umma.

“Maofisa hawa wa Manispaa na Mkurugenzi wao wanatuhumiwa kufanya malipo hewa, ikiwa ni nusu ya fedha zilizotengwa kununua gari hilo, hakika wamefanya kwa makusudi …..: 

“Sasa naomba watupishe ili tufanye uchunguzi kwa kuhusisha vyombo mbalimbali vya dola na wote wawe nje ya ofisi kuanzia sasa, lakini wasitoke nje ya Mji wa Mpanda…..naagiza pia walipe kiasi hicho cha fedha,” aliamuru.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment