Sunday, 27 December 2015

HAYA NDIYO YALIYOSEMWA NA RIDHIWANI KIKWETE WAKATI AKIKANUSHA KUHUSIKA NA MAKONTENA YA BANDARINI NA BIASHARA ZINGINE LUKUKI

Ridhiwani Kikwete

Familia ya Rais wa awamu ya nne Dk Jakaya Kikwete kupitia Mbunge wa Chalinze,  Ridhiwani Kikwete,  ambaye ni mtoto wa rais huyo mstaafu imetoa kauli baada ya mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari kuihusisha na tuhuma za upitishaji makontena bandarini bila kulipiaa kodi.

Ridhiwani alisema tangu serikali ya awamu ya tano ianze kuwabana  watu wanaokwepa kodi za serikali, baadhi ya watu wanafanya jitihada za kumhusisha  yeye binafsi na familia yake na tuhuma hizo.

 “Kama kuna mtu mwenye ushahidi autoe hadharani mimi niuone,dunia iuone, nawahakikishia ushahidi huo haupo na hautokuwepo labda uwe wa kughushi na wakifanya hivyo wataumbuka,” alisema.

Amekanusha pia madai yanayotolewa na aliowaita wapinzani wake kwamba kwamba ana miliki biashara nyingi nchini, yakiwemo maghorofa, mabasi, maroli, vituo vya mafuta na yadi za kuuzia magari.

“Sina na sijawahi kumiliki lori au basi katika maisha yangu.Sina hisa wala ubia na mtu yeyote  au kampuni ya malori au mabasi.” Alisema Ridhiwani

“Naambiwa hapa nchini siku hizi kila jengo jipya linalojengwa inasemekana ni langu na vituo vipya vya mafuta naambiwa ni vyangu, huo ni uongo mtupu, ” alisema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment