Monday, 14 December 2015

HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI YAPATA MWENYEKITI MPYABaraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya la Mufindi limemchagua  Diwani Festo Elia Mgina kutoka kata ya Mninga kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na Diwani Ashery John Mtono kutoka kata ya Sadani kuwa Makamu Mwenyekiti.

Akitangaza matokeo ya Uchaguzi wa baraza la madiwani, Mwenyekiti wa uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Allan Mwela, amesema jumla ya wapiga kula walikuwa 39 ambapo Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti walichaguliwa kwa kula 38 kwa kila mmoja huku mjumbe mmoja hakuweza kupiga kura.

 Akitoa shukran mara baada ya kutangazwa kwa matokeo, Festo Mgina amewashukuru Madiwani wote kwa kumchangua na amewaomba wampe ushirikiano katika kutekeleza majukumu huku akiwaahidi kuwatumikia kwa uaminifu, kuzingata kanuni na taratibu ili kuleta maendeleo ya kweli kwa wana Mufindi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Juma Masenza amewataka madiwani hao kuhakikisha watumishi wote waliopo katika kata zao hususani watendaji wa kata na vijiji wanafanya kazi kwa uadilifu na kwa juhudi ili kutimiza dhana ya uwajibikaji na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ili kukomesha tabia ya kupokea mishahara inayotokana na kodi za umma pasipo kuwajibika.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment