Wednesday, 16 December 2015

EDWARD LOWASSA KUANZA ZIARA YA KUWASHUKURU WATANZANIA NCHI NZIMA


ALIYEKUWA mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amepanga kuanza ziara nchi nzima ya kuwashukuru watanzania kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Taarifa  kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imesema kiongozi huyo atatoa shukrani zake kwa wananchi na jinsi wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani.

Katika ziara hiyo, Lowassa atambatana na viongozi waandamizi wa Chadema na Ukawa kuwashukuru wananchi kwa namna walivyounga mkono upinzani na ajenda nzima ya mabadiliko katika Uchaguzi Mkuu uliopita akianzia Tanga kesho.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment