Thursday, 10 December 2015

DOKTA MAGUFULI ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI, YUPO BALOZI MAHIGA


Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  leo  ametangaza baraza lake la Mawaziri ambalo litakuwa na Mawaziri  19 huku baadhi ya Wizara akisema hazitakiwa na Manaibu Waziri.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Magufuli amesema zilitengwa bilioni 2 kwa ajili ya semina elekezi kwa mawaziri hao; fedha alizomesema zitatumika kwa shughuli zingine za maendeleo kwa kuwa semina hiyo haitakuwepo na kuwataka mawaziri hao wajifunze mambo ndani ya wizara zao.

Alisema wizara zitakuwa 18 lakini Mawaziri ni 19 kwa sababu wizara ya Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma ameiunganisha na Utawala bora hivyo itakua na mawaziri wawili. Wizara ni kama ifuatavyo;

1.       Ofisi ya Rais, Tamesemi utumishi na utawala bora, Mawaziri; Simbachawene na Kairuki, Naibu waziri Jaffo Selemani Said

2.      Osifi ya Makamu wa Rais Mazingira: Waziri ni  January Makamba, naibu  ni  Luhanga Mpina

3.      Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
            Waziri ni Jenista Mhagama, Naibu waziri ni Dk.Posi Abdallah & Antony     Mavunde

4.     Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi : Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba na Naibu ni William Ole Nasha.

5.      Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri Eng. Edwin Ngonyani.

6.      Fedha na mipango: Waziri bado, naibu Dk. Ashantu Kijaji.

7.      Nishati na madini: Waziri ni Prof.Sospeter  Muhongo, Naibu ni  Dk. Medard Kalemani

8.      Katiba na sheria: Waziri ni Harrison  Mwakyembe.

9.     Waziri wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa Dk. Augustine Mahiga  Naibu  wake  Dk. Suzan Kolimba


10.  Ulinzi na kujenga taifa: Waziri Dr. Hussein Mwinyi naibu bado

11.   Ardhi na maendeleo ya makazi: Waziri ni Wiliam Lukuvi, Naibu Angelina Mabula

12.  Utalii: Waziri bado Naibu ni  Eng. Ramo Makame

13.   Viwanda na biashara: Waziri Charles Mwijage

14.  Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi : Waziri bado, Naibu ni Stella             Manyanya

15.  Afya na Ustawi wa jamii: Ummy Mwalimu, Naibu ni Dk.Hamis  Kingwangala

16.  Wizara ya Habari ,Utamaduni na Wasanii : Waziri ni Nape Nnauye,Naibu ni Anastazia Wambura.

17.   Wizara ya maji na umwagiliaji: Waziri Makame Mbarawa, Naibu ni Eng. Isaack Kamwele.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment