Thursday, 17 December 2015

DK MASABURI AFUTA KESI YA KUPINGA USHINDI WA KUBENEA


Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Didas Masaburi amekubali yaishe baada ya kuamua kufuta kuifuta kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo yaliyompa ushindi mnono mwanahabari, Saed Kubenea.

Maombi  ya  kufutwa  kwa  kesi hiyo  yaliwasilishwa  mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam na wakili wake, Clement Kihoko.

Pamoja na kuwasilisha ombi la kuifuta kesi hiyo, mahakama hiyo chini ya Jaji Lugano Mwandambo ilimwamuru Dk Masaburi kulipa nusu ya gharama za kesi kwa mlalamikiwa (Kubenea).


Katika uchaguzi huo  Saed Kubenea alitangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo baada ya kuvuna kura 87,666 na kumwacha kwa mbali mpinzani wake, Dk Masaburi aliyepata kura 59,514.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment