Thursday, 17 December 2015

COCO BEACH, BARABARA ZA CHINI YA KIWANGO ZAMKAANGA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA KINONDONI

Mhandisi Mussa Natty ambaye (‪Pichani‬) kabla ya kuhamishiwa wilayani Babati alikua mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Mussa Natty.

Kabla ya kuhamishiwa Babati, Natty alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Sagini alitangaza uamuzi huo jijini Dar es Salaam jana na kuagiza mkurugenzi huyo kurejea jijini Dar es Salaam.

“Pamoja na kusimamishwa kazi, Natty anapaswa kurudi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na kusubiri uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili. Tuhuma zinazomkabili Natty ni pamoja na usimamizi mbaya uliosababisha barabara za Manispaa ya Kinondoni kujengwa chini ya kiwango na kutochukua hatua kwa watendaji wa manispaa waliokuwa chini yake.

Tuhuma nyingine ni ukosefu wa uadilifu katika ubinafsishaji wa eneo la ufukwe wa bahari eneo la Coco Beach na malalamiko ya wananchi juu ya viwanja katika eneo la Kinondoni, ulioambatana na usimamizi duni wa watumishi hasa sekta ya mipango miji na ardhi” alisema Sagini

Reactions:

0 comments:

Post a Comment