Friday, 4 December 2015

CHINA YAISADIA TAZARA MEBEHEWA 18, VICHWA VINNE VYA TRENI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Judith Kapijimpanga,wakikagua mabehewa hayo.


Serikali ya watu wa China imelikabidhi shirika la Reli Tanzania na Zambia(TAZARA) mabehewa 18 pamoja na vichwa 4 kwa lengo la kuongeza ufanisi katika  utoaji wa huduma za usafiri nchini na Zambia.

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jijini  Dar es salaam mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka, Balozi wa Zambia nchini Tanzania Judith Kapijimpanga  pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing.


Shirika hilo  limepokea msaada huo huku kukiwepo na migomo ya mara kwa mara ya wafanyakazi wake inayosababishwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutolipwa mishahara kwa wakati pamoja na stahiki zingine, mambo yanayopunguza ufanisi wake.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment