Friday, 13 November 2015

WATUMISHI WANNE HALMASHAURI YA HAI WADAIWA KUKWAPUA MILIONI 70


HALMASHAURI ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imewasimamisha kazi watumishi wake wanne kwa tuhuma za kughushi hati za mishahara na nyaraka zilizofanikisha kuchukua jumla ya sh Mil 73.4 zikiwemo fedha za malipo ya muda wa kazi wa ziada kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali teule ya Machame.

Tuhuma hizo zinamtaja Mweka Hazina wa Hosptali hiyo anayedaiwa kushirikiana na watumishi wa halmashauri hiyo kufanya ubadhirifu wa fedha hizo na kwamba tayari uongozi wa hosptali hiyo iliyo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Kaskazini , umekwisha  mfukuza kazi.

Watumishi wawili kati ya wanne wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbili tofauti, moja ni kughushi hati za mishahara, vitambulisho na sahihi za watumishi  waliostaafu  na wengine kuacha kazi na kuchukua mkopo wa Sh Milioni 35 katika benki ya CRDB kwa majina ya watumishi walioacha kazi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment