Friday, 13 November 2015

UKEKETAJI WAPUNGUA NGORONGORO

IMG_0842

Na Mwandishi wetu, Loliondo
IDADI ya wanawake wanaokeketwa Loliondo wilaya ya Ngorongoro imepungua kwa asilimia 75 kwa mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto, Loliondo, Bi. Nailejileji Joseph katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii kwenye warsha ya wiki moja ya mafunzo juu ya Elimu ya Afya ya Uzazi na Maadili.

Warsha hiyo inajumuisha wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii.

Wadau hao wanatoka ngazi mbalimbali ya vitongoji, vijiji na wilaya.
Lengo la warsha hiyo ni kujifunza namna ya kufanya kazi shirikishi ili kuleta mabadiliko sahihi katika jamii inayofanyika katika hoteli ya Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.

Bi Nailejileji alisema idadi ya ukeketaji Loliondo inaonyesha kupungua hadi kufikia 57% mwaka 2015 ikilinganishwa na 87% mwaka 2014 kwa wanawake waliojifungulia hospitalini.

Alisema kwamba matokeo hayo yamefanikiwa kutokana na mkakati maalum unaofanyika shuleni kwa kuanzisha vituo vya kirafiki kwa vijana vinavyolenga kutoa elimu na hamasa kuhusu masuala ya ukeketaji.

Aidha mafanikio hayo ni miongoni mwa jitihada za Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kueneza hamasa shirikishi katika jamii, kuelezea ukubwa wa tatizo, athari zinazotokana na ukeketaji kwa kuwashirikisha wazee wa kimila wa jamii ya Kimasai (Laigwanan) kuchukua hatua zipasazo kukomesha ukatili huu dhidi ya wasichana.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment