Wednesday, 11 November 2015

SAMWELI SITTA, EMMANUEL NCHIMBI WAJITOSA USPIKA


Samweli Sitta na Dk Emanuel Nchimbi ni miongoni mwa makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliojitokeza katika ofisi ndozo za CCM Lumumba hii leo na kuchukua fomu za kuwania uspika wa Bunge la 11.

Sitta ambaye aliwahi kuwa spika wa bunge la 9 na Mbunge jimbo la Urambo kwa miaka 30 na Dk Nchimbi aliyekuwa Mbunge wa Songea Mjini na Waziri wa Mambo ya Ndani, walichukua fomu hizo na kuzirejesha kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Mohamed Seif Khatib.

Wengine waliochukua fomu hizo na kuzirejesha ni pamoja na Banda Sanoko, Dk   Mussa Muzamil Kalokola na Gosbert Blandes.Reactions:

0 comments:

Post a Comment