Monday, 16 November 2015

CCM YAMPITISHA JOB NDUGAI KUGOMBEA USPIKA


Mbunge Mteule wa Kongwa mkoani Dodoma, Job Ndugai, amepitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea Uspika baada ya wagombea wenzake wawili Abdula Ali Mwingi na Tulia Ackson Mwansasu kudaiwa kujitoa.

Ndugai alikuwa Naibu Spika wa bunge lililomalizika muda wake, akimsaidia Anne Makinda ambaye hivikaribuni alitangaza rasmi kujitoa kwenye ulingo wa kisiasa.

Wakati Ndugai akipendekezwa na chama chake kuwania nafasi ya muhimili huo wa nchi, macho na masikio ya watanzania yanasubiri kuona na kusikia ni nani atakayeteuliwa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwania nafasi hiyo.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment