Tuesday, 17 November 2015

BOMU NDILO LILILOFUMUA NDEGE YA URUSI


URUSI imesema kwamba ndege yake iliyoanguka katika rasi ya Sinai ilitegewa bomu lililoisambaratisha ikiwa hewani.

Ndege hiyo ilianguka wiki mbili zilizopita iliua watu wote 224 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Mkuu Idara ya usalama ya  urusi, Alexander Bortnikov,  alisema kwamba bomu lililotegwa katika ndege hiyo lilipuka mara tu baada ya ndege hiyo kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Sharm el-Sheikh.

“Ndege hii ilisambaratishwa angani , ndio maana vipande vyake vilitawanyika sana,” alisema Bortnikov.

Toka wakati ndege hiyo ilipolipuliwa Oktoba 31 mwaka huu safari za ndege kutoka urusi kwenda Misri na za Misri kwenda Urusi zilizifungwa kwa ajili ya usalama.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment