Sunday, 4 October 2015

MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI AJALINIMwenyekiti wa Chama cha DP nchini Tanzania mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia asubuhi  ya leo hii katika ajali ya gari iliyotokea  katika Kijiji cha Msolwa karibu na mji wa Chalinze, kilomita 15  kutoka Chalinze barabara ya Morogoro mkoani Pwani

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Jafar Ibrahim amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema  watu wengine watatu waliokuwa katika gari hilo wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

“Kwa maelezo ya dereva, gari ndogo aina ya Salon waliyokuwa wanasafiria iliacha njia wakiwa wanaelekea jijini Dar es salaam, ikapinduka. Ilikuwa na watu wanne akiwemo dereva na mchungaji Mtikila. Hawa watatu ni majeruhi na mchungaji Mtikila inasemekana amefariki, mwili wa marehemu na majeruhi wamekimbizwa hospitali ya Tumbi,” alisema Kamanda Ibrahim.

Mchungaji Mtikila ni mmoja kati ya wanasiasa  waliochukua fomu ya kugombea urais makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka huu.

Mtandao huu utakujulisha zaidi kuhusiana na tukio hili.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment