Thursday, 29 October 2015

KAULI YA MAREKENI BAADA YA KUFUTWA KWA UCHAGUZI MKUU WA ZANZIBAR


Siku moja baada ya tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais pamoja na wajumbe wa bunge la wawakilishi visiwani humo mataifa ya nje yameanza kuingilia kati suala hilo.

Taarifa  iliyowekwa kwenye mtandao wa ubalozi  wa Marekani nchini Tanzania imeonesha kulaani na  imeshtushwa hatua yaTume ya Uchaguzi kufuta uchaguzi huo huku iki itaka tume hiyo iondoe tamko la kufuta  uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha alisema baadhi ya makamishna wa tume hiyo, badala ya kutekeleza majukumu yao inavyotakiwa kikatiba “wamekuwa ni wawakilishi wa vyama vyao”.

“Kumegundulika kasoro nyingi katika uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kubainika kwa baadhi ya vituo hasa Pemba vimekuwa na kura nyingi kuliko daftari la wapiga kura wa kituo husika.”Alisema Jecha

Alisema hilo ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kwamba “baadhi ya wapiga kura hawakwenda kuchukua vitambulisho vyao vya kupigia kura”.

Aidha, taarifa ya ubalozi wa Marekani imesema kufuta  matokeo hayo kunasitisha mchakato wa uchaguzi uliofanyika vizuri na kwa amani.

Katika hatua nyingine taarifa hiyo imebainsha  kuwa hatua hiyo ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar inakwenda kinyume kabisa na tathmini ya waangalizi wa uchaguzi kutoka ubalozi wa Marekani, jumuiya ya ulaya, jumuiya ya madola na jumui ya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment