Thursday, 29 October 2015

DK MAGUFULI ASHINDA KITI CHA URAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Mgombea Urais wa CCM Dkt.John Pombe Magufuli.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk.John Pombe Magufuli ametangazwa mshindi wa kiti cha urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo, 2015-2020.

Akitangaza matokeo hayo jioni hii Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Damiani Lubuva amesema kati ya wapiga 23,161,440 walioandikishwa, wapiga kura 15,589,639 sawa na asilimia 67.31, walipiga kura.

Alisema kati ya kura hizo zilizopigwa, kura halali zilikuwa 15,193,862 sawa na asilimia 97.46. Kura zilizokataliwa ni 402,248 sawa na asilimia 2.58.

Kwa upande wa matokeo ni kama ifuatavyo;

Anna Mghwira ACT- Wazalendo  amepata kura 98,763 sawa na  asilimia 0.65

Chifu Yemba ADC-Kura 66,049 sawa na asilimia 0.43

Dkt Magufuli John Pombe CCM amepata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46

Edward Lowassa Chadema   amepata kura 6,072,848 sawa na asilimia39.97

Hashim Rungwe Chauma  amepata kura 49,256 sawa na asilimia 0.32

Kasambala Maliki NRA amepata kura 8028  sawa na asilimia 0.05

Lyimo Macmillani TLP amepata kura 8,198 0.05

Dovutwa Nassoro  UPDP amepata kura 7,785 Sawa na asilimia 0.05

Hivyo basi Jaji Lubuva alisema kufuatia kura hizo mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli ametangazwa kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais kwa miaka mitano ijayo kuanzia tarehe atakayoapishwa.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment