Friday, 30 October 2015

DK MAGUFULI AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI WA KITI CHA URAIS


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva leo amemkabidhi mgombea wa CCM Dk John Pombe Magufuli cheti cha ushindi wa urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili (Oktoba 25, 2015).

Dk Magufuli alitangazwa jana kuwa mshindi wa uchaguzi huo baada ya kuwazidi kwa kura wagombea wengine akiwemo Mgombea kupitia UKAWA, Edward Lowassa.


Hafla hiyo ya kukabidhiwa cheti hicho imefanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Upanga jijini Dar es salaam  ambapo wageni mbalimbali walihudhuria akiwemo mwangalizi kutoka nchini Nigeria Goodluck  Jonathan.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment