Monday, 7 September 2015

WAWILI WADAIWA KUPOTEZA MAISHA MKUTANO WA MAGUFULI MOROGORO


WATU wawili wamepoteza maisha baada ya kutokea msukumano na mkanyagano katika mkutano wa mgombea Urais  wa Chama cha Mapinduzi Dk John Pombe Magufuli, uliofanyika jana mjini Morogoro.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dk Ritha Lyamuya amesema mbali na watu hao wawili, wengine 19 walifikishwa katika hospitali hiyo wakiwa wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao.

Alisema kati ya majeruhi hao 19, majeruhi 1o wamelazwa hospitalini hapo huku wengine saba wakiruhusiwa kurejea makwao baada ya kupatiwa matibabu na hali zao kuuonekana kuimarika.

Taarifa za awali zinaonesha kwamba msukumano na mkanyagano huo, ulitokea wakati maelfu ya wananchi wakitoka katika uwanja wa Jamuhuri ulikofanyika mkutano huo.


Mapema leo Rais Jakaya Kikwete aliyehudhuria pia mkutano huo, aliwatembelea majeruhi hao, hospitalini hapo na kuwapa pole 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment