Monday, 7 September 2015

WATUMIAJI WHATSAPP WAFIKIA MILIONI 900


WATUMIAJI wa WhatsApp sasa wamefikia milioni 900 baada ya ongezeko la watu milioni 100 lililofanyika miezi mitano iliyopita.

"WhatsApp sasa ina watumiaji milioni 900," anasema mmoja wa waasisi wa WhatsApp, Jan Koum katika posti yake ya Facebook .

Februari mwaka jana, WhatsApp iliununuliwa na mtandao wa kijamii wa Facebook, kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 19.

Katika post hiyo,Koum  alimtagi pia Ofisa Mtendaji mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg, ambaye pia alijibu kwa kumpa pongezi kwa mafanikio hayo.


Pia mtendaji mwingine wa Facebook, Sheryl Sandberg alimpongeza Koum kwa mafanikio hayo yanayowezesha watu milioni 900 kusalimiana na kubadilishana fikira na kuwachekesha wengine.


WhatsApp imesema kwamba huduma zake zina nguvu sana katika nchi zinazoendelea kama Brazil, India na Russia.

Novemba mwaka jana, WhatsApp imesema kwamba India ina watu milioni 70 wanaotumia mara kwa mara huduma zake ikiwa ni moja ya kumi ya watumiaji dunaini.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment