Thursday, 10 September 2015

VIFAHAMU VIPAUMBELE VYA SERIKALI YA MAGUFULI


Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi Dkt.John Pombe Magufuli   endapo atafanikiwa kushinda  katika uchaguzi mkuu ujao. Hivi ndivyo vitakuwa vipaumebele vyake.
Ajira
Serikali ya Mafuguli imebainisha kuwa itahakikisha kuwa  inawainua kiuchumi wananchi  kwa  kuimarisha viwanda ili kuongeza ajira.
Wamachinga, Mama lishe
Serikali italinda maslahi ya makundi hayo ikiwemo kutowabughuzi, huku akiwataka  mgambo kutafut kazi nyingine kwa kuwa ni kikwazo kikubwa kwao.
Wakulima
Kuboreshewa  maslahi  ya wakulima kwa kuwakopesha sio serikali iwakope.
Wasanii /wanamichezo
Ataanzisha mfuko wa wasanii na  kulinda maslahi yao.
Muungano
Atahakikisha kuwa  watanzania wanakuwa wamoja kati ya Visiwani na Zanzibar.
Ulinzi/Usalama
Ataimarisha ulinzi ili Taifa liwe imara muda wote
Mipaka na Mihimili ya Dola
Atahakikisha Bunge linakuwa imara na lenye kuibana serikali kwa maslahi ya umma.
Mafisadi
Ataanzisha mahakama kushughulikia mafisadi
Madini
Serikali yake itahakikisha kuwa  madini yana nufaisha Watanzania.
Maji
Atahakikisha  maji  yanapatika  vijijini  kwa  asilimia 85 na mjini asilimia 95
Afya
Atajenga zahanati kila kijiji,kituo cha Afya kila kata.
Elimu
(a)Elimu ya Msingi na Sekondari
Serikali itatekeleza  sera mpya ya elimu ambayo ni kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari kidato cha nne pamoja na kujenga nyumba za walimu
(b) Elimu ya Juu
Ata ondoa  uwepo wa Migomo kisa  mikopo kuchelewa, atajenga Hosteli nchi nzima
Wafanyakazi /Walimu
Ataboresha  Masalahi  walimu na  wafanyakazi,atahakikisha kuwa  hakuna mfanyakazi anaingia saa 4 na kutoka saa tano.
Gesi Asilia
Atahakiksha kuwa anasimamia vizuri gesi ya asili ili ihudumie wanachi wote.
Barabara
Ataunganisha Barabara mikoa yote kwa lami, atajenga Fly Overs nyingi ikiwamo Tazara yenye urefu wa k.m 12. Litajengwa daraja kandoni mwa Daraja la Salender Km 7.2, zitajengwa  barabara  za  njia  sita hadi Chalinze na Kisha hadi Morogoro Fly-Over saba.
Reli, Barabara, Ndege
Serikali itajenga Reli ya kisasa maeneo mbalimbali   nchini ikiwamo Dar-Tabora,Mwanza,Mtwara,-Songea Mbambabay,Tanga-Arusha-Musoma na Kaliua-Mpanda.
Mali Asili
Watumishi wa Mali Asili ataboresha maslahi yao ili wachunge tembo kama wasukuma wanavyochunga Ng’ombe ili kuvutia watalii wengi zaidi.
Wafanyabiashara
Atahakikisha analinda maslahi ya wafanya biashara wakubwa na wadogo ili kufanikisha kazi zao na kuchangia uchumi.
Walemavu
Serikali yake italinda Maslahi ya Walemavu.
Wanahabari
Serikali yake italinda uhuru wa Habari na kuwataka waandishi wa Habari kufanya kazi kwa weledi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment