Wednesday, 9 September 2015

UWANJA MPYA WA CHELSEA UTAKAVYOONEKANA BAADA YA KUJENGWA UPYA

Chelsea's New Stadium Will Be A Dark Fortress Of Football

ChelseaStadium2.jpg

UTAKAPOKARABATIWA kwa zaidi ya Pauni za Kingereza Milioni 500, uwanja wa klabu maarufu ya jijini London ya Chelsea FC, the Stamford Bridge, utakuwa ukionekana hivi huku kiwa na uwezo wa kuwaketisha kwenye siti mashabiki wa soka wasiopungua 60,000.

Hivisasa, uwanja huo uliopo Fulham London, una uwezo wa kuchukua mashabiki 41, 798 jambo linaloufanya uwe uwanja wa tisa kwa ukubwa nchini Uingereza.

Viwanja vinavyoongoza kwa kuchukua mashabiki wengi kabla ya Chelsea na idadi yake kwenye mabano ni Wembley (90,000), Old Trafford (75,653), Emirates (60,260), City of Manchester (55,097), St James Park (52, 338), Stadium of Light (48,707), Anfield (44,742) na Villa Park (42,660).

Reactions:

0 comments:

Post a Comment