Monday, 7 September 2015

TRA KUWASHUKIA WAFANYABIASHARA WA VAT WASIOTUMIA MASHINE ZA RISITI


Mamlaka ya Mapato Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu kusni imewakumbusha wafanyabiashara wote waliosajiliwa kwa kodi ya ongezeko la thamani  (VAT) kujiepusha na mkono wa sheria kwa kutumia mashine za kutolewa risiti (EFDA).

Akizungumza na wanahabari hivikaribuni, Mwanasheria wa TRA wa kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Juma Kisongo alisema wafanyabiashara hao wanatakiwa kurumia mashine hizo kwa kuzingatia matakwa ya sheria mpya ya VAT mwaka 2014 iliyoanza kutumika Julai Mosi, mwaka huu.

Alisema maofisa wa mamlaka hiyo watafanya ukaguzi wa kushitukiza katika maeneo ya biashara na kwamba mtu yoyote atakayebainika kuwa hana mshine ya hiyo ama anayo lakini haitumii atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa  mahakamani.

“Utekelezaji wa sheria hiyo umeanza, hivikaribuni kuna mfanyabiashara mmoja alikutwa na tuhuma ya kutotumia mashine ya kutolewa risiti, tulimfikisha mahakamani na amehukuwamia kifungo cha miezi minne au kulipa faina ya Sh 400,000,” alisema bila kumtaja mfanyabiashara huyo.

Alisema pamoja na kupewa adhabu hiyo, mahakama hiyo imempa mfanyabiashara huyo hadi kufikia mwezi huu awe amenunua na kuanza kutumia mashine hiyo.

Alisema TRA inafahamu uwepo wa baadhi ya wafanyabiashara waliosajiliwa kulipa VAT kukwepa kutumia mashine hizo na hata wanapozitumia wamekuwa wakiwaomba wateja kuandika pungufu ya bei halali za mauzo ya bidhaa na huduma.

“Tunapenda kutoa wito kwa wafanyabiashara hao watumie mashine hizo na wasifanye ujanjaujanja; vile vile kwa wale wote ambao mauzo yao yanafikia Sh 14 milioni kwa mwaka nao nao ni muhimu wakatumia mashine hizo ili waweze kupata makadrio sahihi ya kodi zao” alisema.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA Mkoa wa Iringa, Faustne Masunga aliwataka wafanyabisha wote ambao huchukua tenda serikalini kuwa na mashine hizo za kutolea risiti.

Alisema utaratibu wa serikali unazuia kuingia mkataba na kampuni au mfanyabiasha asiye na mashine ya kutolea risiti.

“Nitoe wito kwa wafanyabishara wote na hasa kampuni ambazo huingia mkataba wakufanya kazi na serikali, baada ya sheria hii kupitishwa hakuna kampuni wala mfanyabiushara atakayeingia mktaba wa kufanya kazi na serikali bila ya kuwa na mashine ya kutolea risti” Masunga alisema.

Katika hatua nyingine Masunga aliwataka wananchi kudai risiti pindi wanaponunua bidhaa ili kuisaidia serikali kupata mapato lakini pia kulinda bidhaa zao na hofu ya kuwa ni za wizi.

“Ikiwa mtu atanunua bidhaa na kuondoka nazo bila kupatiwa risiti anaweza kukamtwa na kudaiwa ni za wizi na kama atakuwa na risti itamsaidia kulinda bidhaa alizonunua na atakuwa amesaidia serikali kupata mapato” alisema.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment