Wednesday, 23 September 2015

TIGO WASAIDIA MADAWATI 400 IRINGA VIJIJINIKAMPUNI ya huduma ya simu za mkononi ya Tigo mjini Iringa, imekabidhi msaada wa madawati 400 kwa halmashauri ya wilaya Iringa yatakayowezesha kupunguza upungufu wake katika shule zake.

Msaada huo wenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 28 umetolewa na kampuni ya Hassan Maajar Trust kupitia kampuni hiyo ya simu nchini.

Akishukuru kwa msaada huo uliokabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Pudensiana Kisaka alisema kabla ya kupokea madawati hayo halmashauri yake ilikuwa na upungufu wa madawati 9,392.

“Wakati mahitaji kwa shule zetu za awali na msingi ni 27,246 tuliyonayo ni 17,854 tu, takwimu hiyo inaonesha jinsi tulivyo na upungufu mkubwa,” alisema.

Alisema msaada huo toka Tigo utawezesha wanafunzi 1,200 kuondokana na adha inayosabbabishwa na upungufu wa madawati katika shule zao zenye jumla ya wanafunzi zaidi ya 67,000.

Akielezea juhudi zao katika kukubalina na changamoto mbalimbali za kimaendeleo ndani ya halmashauri hiyo, Kisaka alisema wamekuwa wakishirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo kampuni hiyo ya Tigo katika kupambana na changamoto zinazowakabili.

Ili kuboresha mazingira yatakayowawezesha wanafunzi wa wilaya hiyo kupata elimu bora, Afisa Elimu Wilaya ya Iringa wa Shule za Msingi, Selemani Pandawe aliwaomba wadau wengine wajiitokeze kuisadia sekta hiyo.

Akiongea kabla ya kukabidhi madawati hayo Mkurugenzi wa Tigo wa Kanda wa Tigo Jackson Kiswaga alisema kampuni ya wametumia fursa waliyoipata kutoka kampuni ya Hassan Majaar Trust kuwasaidia wananchi wa halmashauri hiyo.

Alisema msaada huo unaimarisha mazingira rafiki ya waomba kusadia Madawati kiasiwalicho weza kwa awamuhii ilikupunguza ukubwa wa uhitaji uliopo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa aliwataka walimu na wanafunzi wa shule zilizonufaika na msaada huo kuyatunza il yawanufaishe wengi zaidi kwa muda mrefu zaidi.

Alisema vipo baadhi ya vifaa vya shule katika shule mbalimbali mkoani humo vimeharibiwa kwa makusudi na hivyo kuitia hasara kubwa serikali na wadau wake wenye nia njema katia kuiboresha sekta hiyo.

Alisema ni muhimu kwa bodi za shule kujiwekea utaratibu utakaotoa adhabu kwa wanaoharibu mali za shule kwa makusudi na akapendekeza moja ya adhabu hizo kuwa ni kuwalazimisha wahusika wenyewe au kwa kupitia wazazi au walezi wao kulipa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment