Monday, 28 September 2015

SHAKIRA AKIRI UMAMA MGUMU


MWIMBAJI mashuhuri duniani Shakira katika siku za karibuni amekiri kwamba kazi ya kuwa mama si masihara na ni kazi ngumu ambayo hajawahi kuifanya katika maisha yake .

Akizungumza na PEOPLE alisema amekuwa siku zote akitafuta taarifa zaidi jinsi ya kuwa mama bora kupitia mtandao wa kijamii, akisoma na kutafiti.

Amesema si rahisi kuwa mama kwani katika maisha yake ni moja ya shughuli ngumu kabisa aliyofanya duniani.

Alisema alishakuwa katika wakati mgumu wa kuwaburudisha wapenzi wake, kukutana na viongozi wa kitaifa na kimataifa, lakini hajawahi kujitambua kama kujishughulisha na suala la kuwa mama.

Amesema kila siku anajiuliza kama anafanya vyema kwa ajili ya watoto wake.”ninataka kuboresha zaidi kazi hii ngumu duniani, kazi ya kuwa mama” alisema mwimbaji huyo wa Colombia ambaye ana watoto wawili kutoka kwa mshirika wake mchezaji wa Barca, Gerard Pique


Reactions:

0 comments:

Post a Comment