Monday, 7 September 2015

MWAKALEBELA AFUNIKA IRINGA MJINI, MWIGULU AHOJI SABABU ZA SUMAYE KUWA WAZIRI MKUU KWA MIAKA 10, ATILIA SHAKA AFYA YA LOWASSA

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimezindua kampeni za ubunge jimbo la Iringa Mjini kwa kumnadi mgombea wake, Frederick Mwakalebela katika mkutano mkubwa uliojaza kiwanja cha Mwembetogwa mjini hapa, huku kikisikitika kwanini Frederick Sumaye alikuwa Waziri Mkuu kwa awamu zote mbili za Rais mstaafu, Benjamin Mkapa.

“Tumemleta Dk John Magufuli kwasababu tuna hakika atakuwa kiboko ya wazembe serikalini, wanaochelewesha haki za wananchi. Kuna watu wamepewa majukumu na serikali lakini ni wababaishaji,” alisema aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba wakati akizindua kampeni hizo.

Nchemba alisema wapinzani wao wamekuwa wakikesha kutafuta mapungufu ya Dk Magufuli na kwa kuyakosa wanawahamasisha watanzania wamkatae “tu kwa kisingizio kwamba hawezi kuwa kiongozi bora kwa kupitia mfumo ule ule.”

Alisema inashangaza kuona mtu aliyekuwa waziri mkuu kwa miaka 10 anatoka hadharani na kuwaaambia watanzania kwamba ndani ya serikali ya CCM kuna matatizo.

“Kama kuna matatizo yanayohusu mfumo, utendaji na haki za watu, tukiamua kuwajibishana Sumaye hawezi kupona kwasababu na y eye ni sehemu ya matatizo hayo na ndio maana katika kipindi chake chote hayakwisha ” alisema.

Nchemba alisema amekuwa akijiuliza kwa muda mrefu kwanini Sumaye alikuwa akiitwa jina fulani lisilofaa wakati akiwa madarakani, lakini sasa amezijua sababu zake na anaamini waliomuita hivyo walikuwa sahihi.

“Nilikuwa najiulizaga sana knini mtu huyu alipokuwa waziri mkuu alikuwa anaitwa jina fulani lisilo faa, sasa nimejua jina hilo ni sahihi kweli kweli,” alisema.

Kuhusu Lowassa
Nchemba alisema “Tuweni wakweli, hivi leo CCM ingemsimamisha huyo mgombea wao kuwa mgombea urais wa CCM, wapinzani wangesemaje?...tuache kuwalaghai watanzania kwa maslai binasfi.”

Kabla hajahamia kwao, alisema wapinzani walikuwa wanasema mgombea huyo anastahili kuwa jela na hastahili kuitwa waziri mkuu mstaafu bali anastahili kuitwa waziri mkuu aliyejiudhuru kwa kashfa ya wizi.

Alisema watanzania wanahitaji kutafakari na kuliombea sana taifa ili lipate kiongozi wa nchi atakayeheshimu utawala wa sheria.

“Nawashangaa sana wapinzani, unaorodhesha matatizo kibao na unakiri kweli kuna matatizo, halafu aina ya mtu unayetaka kumleta, ni Rais wa kuania juani mchana kutwa na wakupigapiga betri zilizoisha chaji kama za national.”

Nchemba aliuliza kama ni akili kweli kumchagua Amiri Jeshi Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania atakayelinda mipaka ya nchi ambaye hawezi kuhutubia zaidi ya dakika kumi.

Alisema ipo mikutano ya kimataifa inayoanza saa 4.00 asubuhi na kumalizika saa 5.00 usiku na kwamba katika mazingira hayo litakuwa ni jambo la fedheha kumpeleka Rais ambaye hawezi kuongea kwa zaidi ya dakika 10.

“Rafiki yangu Mchungaji Msigwa aje akanushe, alisema mtanzania yoyote na mwana CCM yoyote atakayemshabikia Lowassa akapimwe akili,”

Alisema mmoja wa watu ambao zamani nilikuwa siwaheshimu alikuwa ni Dk Slaa, lakini kwa mapenzi yake na msimamo wake wa kuita nyeusi ni nyeusi, bereshi ni bereshi na kijiko ni kijiko atakujakumbukwa na vitukuu wetu.

Alisema Lowassa amekuwa akijinasibu kwamba endapo atakuwa Rais wa nchi hii ataendesha nchi kwa kasi kubwa wakati, kusimama, kutembea na kila kitu anachofanya anakifanya kwa kasi ya kinyonga.

Frederick Mwakalebela.
Akimnadi Mwakalebelea kwamba anafaa kuwa mbunge wa Iringa Mjini kwasababu anayajua na kuyashughulikia matatizo ya watu wake, Nchemba alisema Mchungaji Msigwa atakumbukwa kwa hoja zake zilizokuwa zinaichachafya serikali lakini hapaswi tena kurudi bungeni kwasababu ya ukigeugeu.

“Msigwa alikuwa anaisema sana serikali na wiziara ya malisiali na utalii lakini alipoanza kushirikishwa nay eye kwenye manyunyumany na majimaji mazuri, akawa wa kwanza kunyamaza kimya na kunga mkono mambo yote yanayofanyika,” alisema.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alisisitiza kauli yake ambayo amekuwa akiitoa mara kwa mara kwamba Mchungaji Msigwa apende asipende wananchi wa Iringa Mjini wameshamchoka na hatarudi tena bungeni.

Akizoma idadi ya vikao vya kamati ya uchumi na fedha vya manispaa ya Iringa ambavyo Msigwa hakuhudhuria tangu awe mbunge wa jimbo hilo, Mtenga alisema Iringa wanataka mbunge wa Maendeleo na wala sio mbunge wa kubweka.

Akijinadi, Mwakalebela mwenyewe alisema “leo hii CCM mpya imezaliwa, watu walisema haipo leo hii kila aliyefika hapa kashuhudia umati mkubwa wa watu nah ii inaonesha kiu kubwa ya maendeleo mliyonayo baada ya kuikosa kwa miaka mitano iliyopita.”

Alisema anafahamu afanye nini kwa vijana, wafanyabiashara, akinamama, wakulima, wafugaji, makundi maalumu, walimu, wanamichezo na kwa wafanyakazi.

Alitaja vipaumbele vyake endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kuwa ni pamoja na kuboresha huduma za afya, maji, miundombinu, elimu na sekta michezo ambayo aliahidi kufanya kila atakaloweza ili timu ya Lipuli inayoshiriki ligi daraja la kwanza, ipande daraja.  

Akizungumzia changamoto ya vijana kukosa ajira, Mwakalebela alisema atatumia sehemu kubwa ya mshahara na marupuru yake kusaidia vijana bila kuangalia itikadi zao.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment