Monday, 7 September 2015

MGAO WA UMEME NCHINI KUANZA LEO


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetangaza kuwa na ukosefu wa umeme katika mikoa yote inayotumia Gridi ya Taifa kuanzia leo.

Hatua hiyo inatokana na kuzimwa mitambo yote ya umeme katika kituo kikubwa cha kuzalisha umeme cha Ubungo, Dar es Salaam kwa nia ya kuingiza gesi asilia katika mitambo huo.

Mgao huo unadaiwa kuwa utadumu kwa wiki nzima ukihusisha  umeme kukatika kwa saa kadhaa usiku na mchana, lakini hali itakuwa mbaya zaidi kwa siku ya leo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema mitambo yote ya umeme itazimwa ili kuingiza gesi asilia kuanza kuzalisha umeme katika kituo hicho kikubwa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment