Wednesday, 9 September 2015

KUBENEA AIBUA MAZITO YA RICHMOND, AMLIPUA DOKTA SLAA


Hatimaye mwandishi wa Habari mahiri nchini Tanzania Saed Kubenea ambaye pia ni mgombea ubunge jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam amelianzisha upya sakata la Richmond akidai kwamba wakati  likiwakilishwa  bungeni  kulikuwa  na  ripoti  mbili.

Kubenea amesema moja  ya ripoti hizo ililenga  kumchafua Edward Lowassa ambaye ni mgombea urais kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)  na  ya  pili  ikimtaja kiongozi mmoja nchini.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Kubenea alisema kwamba anatarajia kulivalia njuga suala la Richmond na kusisitiza kuweka hadharani kila kitu.

Licha ya kuzungumzia sakata hilo mkoani Mbeya, Kubenea alisema atalizungumzia pia jijini Dar es salaam katika mkutano wake na Waaandishi wa Habari.

Licha ya sakata hilo Kubenea amezungumzia suala la aliyekuwa Katibu wa Chadema Dk Wilbroad Slaa kujiuzulu, akisema aliyekuwa  akipinga  ujio  wa  Lowassa  Chadema  ni  Profesa Baregu  na wala  siyo  Dk Slaa.

Amesema  kamati  kuu  ya  Chadema  ilijiridhisha  kuwa  Dk Slaa  asingeweza  kushinda  uchaguzi  wa  mwaka  huu  kama  angesimamishwa  kuwa  mgombea  wake  urais.

Ameongeza kuwa   “kilichomponza Slaa  ni  mkewe  ambaye  alikuwa na uchu wa kuwa first lady. Ili kufanikisha ndoto hiyo ya mkewe, Dk Slaa  alianza  kampeni  za  kumpinga Lowassa  ili  ateuliwe  yeye,” amedai Kubenea.

Katika kuufanikisha mpango huo, Dk Slaa aliamua kumtuma Sugu  aende Mbeya  akawaambie  waumini wa makanisa yote kuwa wao wanamtaka  Slaa  na  sio  Lowassa, lakini  Sugu  alikataa.

Amesema Slaa  pia  alijaribu  kumrubuni Tundu Lissu  atangaze kumpinga Lowassa  lakini  naye  alikataa  pia  na  kujikuta  akibaki  peke  yake, hali  iliyomfanya  ajivue  uanachana.

Katika kumshambulia Slaa zaidi, Kubenea amesema,  “Slaa  alikuwa Padri  akaasi, alikuwa na mke akaasi, alikuwa CCM akaasi, je ana principle gani za kuwashawishi watanzania  wamuamini?”.

Akizungumzia taarifa ya Dk Slaa kuzipata nyaraka za Richmond toka kwa Dk Harrison Mwakyembe, Kubenea alisema: “Ukweli ni kuwa Mwakyembe hawezi  kuwa mtu sahihi  wa  kutoa  nyaraka  za  Richmond  kwa  sababu  wakati  wa ripoti  hiyo, Mwakyembe  alikuwa na kampuni yake  ya  kufua  umeme  ambayo  alitaka  ipite. Baada  ya  kukwama  ndo  akaanza ugomvi na Lowassa.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment