Monday, 28 September 2015

DK MAGUFULI ATOA AHADI NZITO KWA SALIM ASAS


MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli ameahidi kumpa msaada mkubwa Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Asas (Asas Group of Companies) wa mjini Iringa, Salim Asas; utakaomuwezesha kuwekeza kwenye viwanda ili atengeneze ajira mpya kwa vijana.

Mbali na kampuni yao kuendesha kiwanda cha kusindika maziwa cha Asas Dairies Ltd, kampuni hiyo ina shamba kubwa la ng’ombe na inafanya biashara ya usafirishaji, vituo vya kuuza mauta na inajenga nyumba za kupangisha.

“Lete viwanda vingi nakuhakikishia kukupa ‘support’ kwa asilimia 100. Serikali ya magufuli inataka wawekezaji kama wewe, wanaofanya mambo yanayoinua uchum wa Taifa na kutoa ajira kwa vijana wetu wanaomaliza vyuo vikuu,” alisema.

Kauli hiyo ya Dk Magufuli imepeleka simanzi kwa mpinzani mkubwa wa CCM mjini Iringa, Mchungaji Peter Msigwa ambaye hivikaribuni alinukuliwa akiwahimiza wafuasi wachama hicho na wapiga kura wa mjini Iringa kususia biashara zinazofanywa na kampuni hiyo kwa madai kwamba faida anayotengeneza katika biashara hizo anaitumia kukandamiza ukuaji wa demokrasia.

“Hata ukitaka kutengeneza kiwanda cha Ulanzi, wewe tengeneza tu kwani serikali yangu itakupa msaada unaouhitaji,”  Dk Mafuli alisema kwa msisitizo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alimponda Mchungaji Msigwa anayegombea kwa mara nyingine tena ubunge wa jimbo la Iringa Mjini kupitia chama chake, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akisema anataka ubunge kwa maslai yake binafsi.

Mchungaji Msigwa anayeelekea kupata ushindani mkubwa kutoka kwa mgombea wa CCM, Frederick Mwakalebela alikuwa mbunge wa jimbo la Iringa Mjini kati ya mwaka 2010 na 2015 ambazo Dk Magufuli alisema nyingi kati yake zilikuwa za wana CCM waliokasirika baada ya kusikia jina la Mwakalebela pamoja na kwamba alishinda kura za maoni mwaka 2010,kukatwa.

Itaendelea...........................

Reactions:

0 comments:

Post a Comment