Monday, 28 September 2015

DK MAGUFULI ASEMA SHIDA ZA WATANZANIA HAZINA MAHUSIANO NA UKAWA


MGOMBEA Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli amesema shida za watanzania hazina mahusiano na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) bali ni matokeo ya rasilimali za nchi kutowafikia na kuwanufaisha waliowengi ambao ni wanyonge.

Akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mafinga na vitongoji vyake, jana, Dk Magufuli alisema kama wanyonge wanataka wanufaike na rasilimali hizo, waisthubutu kupeleka mafisadi Ikulu.

“Binafsi najua kama kuna kura sitapata basi ni za majizi na mafisadi ndani na nje ya CCM na serikalini. Kwahiyo mnaotaka mabadiliko nipeni kura za kutosha ili nifunge dhuluma zote kwa jina langu mwenyewe Magufuli,” alisema


Alisema kiu ya watanzania kupata Tanzania Mpya itafikiwa kwa kumchagua yeye kwani anayo dhamira ya dhati ya kushughulikia kero za wananchi wanazopata katika sekta mbalimbali nchini.

Dk Magufuli anayeendelea na kampeni zake mkoani Iringa, leo anatarajia kuhutubia wakazi wa mjini Iringa katika uwanja wa Samora mjini hapa, kabla hajaendelea na ziara hiyo kesho katika vijiji vya Pawaga na Migoli, Jimbo la Isimani.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment