Monday, 28 September 2015

DK MAGUFULI APONGEZA UVUMILIVU WA MWAKALEBRELA AKISEMA UNALIPA


Add caption
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli amemsifu mgombea ubunge jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Frederick Mwakalebela akisema ni mvumilivu mwenye upendo kwa watu wa Iringa.

“Pamoja na kwamba mwaka 2010 alishinda kura za maoni na baaye jina lake kukatwa, Mwakalebela hakuhama chama,” Dk Magufuli alisema wakati akimnadi Mwakalebela kwa wakazi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake waliojitokeza katika mkutano wa kampeni za mgombea huyo wa urais.

Alisema kama Mwakalebela asingekuwa mvumilivu isingekuwa rahisi kwake kupata fursa ya kugombea ubunge katika jimbo hilo mwaka huu.

“Na uvumilivu wake umemfanya aaminike na ndio maana Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Mkuu wa wilaya kabla hajarudi kuomba kwenue ridhaa ya kuwatumikieni, “alisema.

Alisema endapo watamchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo, atatoa ofa ya kujenga barabara nyingine za urefu wa kilomita 10 kwa kiwango cha lami.

Itaendelea………………………….

Reactions:

0 comments:

Post a Comment