Sunday, 13 September 2015

DIWANI AFARIKI KATIKA AJALI YA BARABARANI, ALIKUWA AKIENDESHA BODA BODA


Aliyekuwa diwani wa kata ya KITWIRU MANISPAA ya Iringa, Ally Mbata amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali iliyohusisha pikipiki aliyokuwa akiiendesha na gari ambalo hata hivyo halikuweza kujulikana.

Mbata alipata ajali hiyo wakati akitoka kwenye kampeni za Uchaguzi katika kata ya Ndiuka ambayo ni kata jirani na kata yake ya Kitwiru.

Baadhi ya watu wanaodai kushuhudia ajali hiyo walisema, gari iliyohusika katika ajali hiyo ilitokomea kuelekea njia ya Mbeya, huku taa zake zote zikiwa zimezimwa.

“Marehemu ameumia vibaya kichwani,” alisema mmoja wa mashuda wa ajali hiyo ambaye hata hivyo hakutaja jina lake.

Taarifa zilizotolwa na mdogo wa marehemu Mbata, Hamid Mbata, zinaonesha kwamba marehemu atazikwa jioni ya leo katika makaburi ya Makanyagio, mjini Iringa.

Katika taarifa yake kwa wanahabari, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimepokea msiba huo kwa masikitoko makubwa kwani Mbata aliyekuwa mjumbe wake wa Kamati ya Siasa ya Manispaa ya Iringa alikuwa kiuongo muhimu katika kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazoendelea.

CCM imewataka wana familia, ndugu na jamaa wa marehemu kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu


R.I. P Ally Mbata

Reactions:

0 comments:

Post a Comment