Friday, 14 August 2015

WAZIRI WA MAZINGIRA APIGWA CHINI KURA ZA MAONI MAKETE


MKUU wa wilaya ya Songea, Profesa Norman Sigalla amembwaga Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk Binilith Mahenge katika kura za maoni za marudio ya ubunge jimbo la Mekete.

Wakati Profesa Sigalla alijizolea kura 8,838, Dk Mahenge anayelalamikiwa na wapiga kura wa jimbo hilo kwamba ana mkono wa birika alipata kura 7,885.

Akitangaza matokeo hayo jana, Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Jumanne Kapinga aliwataja wapiga kura wengine na kura zao kwenye mabano kuwa ni Bonike Mhami (124), Fabian Nkinga (74) na Lufunyo Nkinda (42).

Kabla ya matokeo hayo kutangazwa kulikuwepo na taarifa zilizomtaja Dk Mahenge kuyapinga huku akitaka uchaguzi huo katika kata ya Lupila urudiwe tena kwa madai kwamba kulikuwepo na dosari ya uhesabuji.

Kuangushwa katika kura hizo za maoni kumeelezwa na wachambuzi wa kisiasa wa mkoani Njombe kumpa nafasi finyu waziri huyo ya kuendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mingine mitano.

Uchaguzi huo ulirudiwa baada ya Profesa Sigalla kuulalamikia Uchaguzi wa Agosti 1 kwamba uligubikwa na dosari na udanganyifu mkubwa ambao hatimaye ulimpa ushindi Dk Sigalla.

Katika uchaguzi huo wa awali, Dk Mahenge alipata kura 8,534 huku Profesa Sigalla akipata 8,211, Mhami 500, Kingwa 486 na Nkinda 226.

Kwa kile kilichothibitisha kuwepo kwa udanganyifu wa matokeo ya awali baadhi ya wana CCM wa Jimbo hilo walilazimika kusafiri hado makao makuu ya CCM ya waailaaya hiyo wakipinga matokeo hayo kutangazwa.

Dk Mahenge alichaguliwa kuwa mbunge wa Makete kwamara ya kwanza katika uchaguzi mkuu wa 2005 na alishinda tena katika uchaguzi mkuu wa 2015 na hivyo kufanya awe amewatumia wananchi wa Makete kwa miaka 10.

Mmoja wa wananchi wa jimbo hilo, Neston Sanga alisema; “miaka 10 inamtosha, jimbo linahitaji mtu mpya tutakayeshirikiana naye kushughulikia changamoto mbalimbali ikiwemo ya maji ambayo Dk Mahennge alishindwa kuishughulikia alipokuwa naibu waziri wa maji.”

Reactions:

0 comments:

Post a Comment