Sunday, 23 August 2015

WANANCHI WABOMOA NYUMBA YA MGOMBEA UBUNGE WA CUF, NI BAADA YA KUTOKOMEA NA FOMU ZA UBUNGE

Nyumba ya Mgombea urais Twahiri Saidi.

Mgombea Ubunge wa wa chama cha wananchi CUF jimbo jipya la nanyamba wilaya ya Mtwara Vijijini, Twahiri Saidi amebomolewa nyumba yake   na wananchi  wenye hasira kali  baada ya  kushindwa kurudisha fomu ya ubunge na kutokomea kusiko julikana huku akizima simu.

Kwa mujibu wa baadhi ya viongozi wa chama hicho na wanachi wa jimbo la Nanyamba wamesema kutoweka kwa mgombea huyo  kuna dalili ya mchezo mchafu uliotumika kumfanya mgombea wa CCM Abdallah Chikota  kupita bila kupingwa.

Naye katibu kata wa CUF kata ya Milango Minne eneo analotoka mgombea huyo, amesema mwisho wa kuwasiliana na mgombea huyo ilikuwa majira ya saa saba akimuhimiza kuwahisha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi.

Hata hivyo anasema majibu ya mgombea huyo yalionyesha wazi kuna jambo baada ya kudai hawezi kuacha ajira yake na kuingia kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi wakati viongozi wa CUF taifa walimuaidi kumpa shilingi milioni 30 kwa ajili ya uchaguzi na wameshindwa kufanya hivyo.

Jeshi la Polisi mkoani humo limewataka wananchi kuwataja walio bomoa nyumba hiyo vinginevyo mkono wa sheria utachukua mkondo wake.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment