Wednesday, 26 August 2015

UKAWA KUTUMIA VIUNGA VYA JANGWANI KUIJIBU CCM NA KUNADI SERA ZAKE


Mgombea Urais wa UKAWA Edward Lowassa anatarajia kuzindua kampeni siku ya Jumamosi, Agosti 29 katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam sehemu ambayo Chama cha Mapainduzi CCM kilizindua kampeni yake  jumapili iliyopita.

Wagombea waliosimamishwa na umoja huo ni Edward Lowassa ambaye ni mgombea urais na Juma Duni Haji, mgombea mwenza, wote kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wanasiasa wengine kutoka vyama vya upinzani watanatarajia kuhudhuria uzinduzi huo.


Mmoja wa makamanda kutoka ndani  ya UKAWA amesema uzinduzi huo utakuwa wa aina yake huku akisistiza kuwa moja ya makubaliano yao ni kuepuka siasa za matusi na kuahidi kuwa watatumia uzinduzi huo kujibu hoja za wapinzani wao na kunadi sera zao kwa wananchi.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment