Monday, 10 August 2015

PROFESA LIPUMBA AUNDIWA KAMATI

Prof Ibrahim Haruna Lipu

Chama cha wananchi CUF kimeunda kamati ya muda itakayodumu kwa miezi sita ili kusimamia  nafasi za uongozi  na  kuziba pengo la Prof. Ibrahim Lipumba liyejiuzulu  uenyekiti hivi karibuni.

Hayo yamesemwa   muda  mfupi    Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa mkutano na waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika Kikao cha Dharula cha Baaraza la kuu la uongozi wa chama hicho kilichoitishwa kujadili hatua hiyo ya kujiuzulu Profesa Lipumba .

Amesema katokana na Kanuni za CUF wamekubaliana kwa pamoja kuunda kamati maalum itakayosimamia chama kwa kipindi cha Miezi sita na baadae kufanya uchaguzi wa nafasi hiyo ya mwenyekiti.

Ameongeza kuwa  Kamati hiyo itakuwa chini ya Katibu wa CUF ambaye ni yeye Maalim Seif na mwenyekiti wake atakuwa Mbunge wa Afrika Mashariki   Twaha Taslima.


Katika hatua nyingine  Kamati hiyo itakuwa na kazi ya kukijenga chama hicho,pamoja na kushirikiana na Vyama vyengine vinavyounda UKAWA  ambapo anadai itakuwa na jukumu lingine la  kuhakikisha wanaitoa CCM madarakani.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment