Monday, 10 August 2015

MWENYEKITI WA CCM ARUSHA ATIMKIA CHADEMA


Aliyekuwa  Kigogo wa Chama cha  Mapinduzi ambaye ni  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Mh Onesmo Nangole na Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha,Mh. Isack  Joseph  wamejiuzulu nafasi zao zote  na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Wakizungumza   mara baada ya kutua  Upinzani vigogo hao  wamemtaka  Katibu  Mkuu  wa  CCM, Mh Kinana  kuacha  mara  moja siasa  za  matusi za  kuwaita  Makapi  wanachama  ambao  wamekuwa  wakijiunga  na  vyama  vya  upinzani.

Licha ya Vigogo hao kuhamia chadema wanachama wengine zaidi ya mia 300 waliokuwa chama cha CCM kutoka jamii ya kifugaji katika kata ya Engaruka wilaya ya Monduli  juzi  walizichoma kadi zao za CCM na kujiunga na CHADEMA .

Katika hatua nyingine Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye amedai kwamba kumekuwepo na hujuma zinazofanywa na upinzani kwa kuchapisha kadi feki za CCM kisha kupewa wananchi ili waonekane kama kweli wanakihama chama hicho.
Kwa upande wa uongozi wa juu wa Chadema umewataka wananchi wote wanao choshwa na Siasa za CCM kuhamia chama hicho kwa kuwa kila mwananchi ana uhuru wa kuhamia chama chochote cha Siasa  anachokipenda.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment